Serikali ya Kenya imesitisha kazi za kuwapeleka wafanyakazi wa nchi hiyo katika nchi za kiarabu hadi pale serikali imekamilisha uchunguzi na kuhakikisha kuna mfumo wa kulinda maslahi ya raia wake.
Waziri wa kazi wa Kenya Kazungu Kambi, katika hatua nadra amesema amechukua uwamuzi huo kufuatia kuongezeka malalamiko ya Wakenya kunyanyaswa.
Your browser doesn’t support HTML5
Amesema, anasitisha pia kazi zote za mashirika yanayowaajiri watu na kuwapeleka katika nchi za kiarabu kufanya kazi. Anasema wameanza majadiliano na mataifa hayo ya kiarabu ili kuhakikisha kwamba maslahi ya wafanyakazi yanalindwa.
Katibu Mkuu wa chama cha mawakala wa kuajiri wafanyakazi Hussein Adnan, anasema uwamuzi kwa upande moja utaruhusu kuchambua mawakali wa kwlei na wale wa bandia, na utatoa nafasi kupanga utaratibu bora zaidi kufuatilia wafanyakazi wanaopelekwa kufanya kazi katika nchi hizo za Kiarabu.