Viongozi wa vyama vya upinzani nchini Tanzania wanahoji mfumo mzima wa uchaguzi kutokana na tume hiyo kutangaza kupanda kwa gharama za ununuzi wa mashine za kisasa za kuandikisha wapiga kura (BVR) Biometric Voter Registration.
Hayo yalisemwa jumatano katika mkutano kati ya tume ya uchaguzi nchini Tanzania na vyama vya siasa .
Mashine hizo zinatarajiwa kuanza kutumika mwezi Septemba mwaka huu. Akizungumza na idhaa ya Kiswahili ya sauti ya Amerika (VOA) mbunge wa Singida Mashariki kupitia CHADEMA Tundu Lissu amesema wao hawaridhiki na mambo mengi yaliyoelezewa katika mkutano huo, lakini alililotaja ni ile dhana kwamba matatizo ya kimfumo yanaweza kutatuliwa kwa kutumia teknolojia.
Your browser doesn’t support HTML5
Lakini amesema tume nzima ya uchaguzi haiaminiki kwasababu ya matendo yake na ilivyoundwa na inavyofanya kazi akiongeza kwamba tume ya makamishna na wajumbe huteuliwa na rais na maafisa wa tume ni watumishi wa serikali .
Kuhusu UKAWA kurudi bungeni amesema mabadiliko yatapatikana tu hata kama hawarudi bungeni kwasababu wakirudi ni kama kusaidia mfumo mbovu uliopo sasa, aliongeza kwamba watapata katiba mpya kwa njia nyingine na sio hili bunge.
Aliongeza kuwa mapambano yataendelea kwasababu kitakachopatikana kwenye bunge la katiba bila UKAWA kitakuwa hakina uhalali wa kisiasa ingawa kinaweza kuwa na uhalali wa kisheria lakini wananchi wengi hawatakikubali.