Mawakili wa utetezi wakamilisha kutoa hoja kwenye kesi ya Pistorius.

Oscar Pistorius akisikiliza kesi yake mahakamani Pretoria, Afrika kusini. May 14, 2014.

Timu ya utetezi ya mwanariadha wa Afrika kusini Oscar Pistorius imemaliza kuwasilisha utetezi wao katika kesi ya mauaji na kubakisha maelezo ya mwisho kabla ya jaji kutoa uamuzi wake.

Wakili Barry Roux aliiambia mahakama jumanne kwamba amemwita shahidi wake wa mwisho.

Jaji Thokozile Masipa aliahirisha kesi hiyo mpaka Agosti 7 na 8, wakati mahakama itakaposikiliza maelezo ya mwisho.

Pande zote mbili zitatoa maelezo yao mapema na Masipa alisema jumanne hakuna yatakayowekwa hadharani mpaka yatakapowasilishwa mahakamani.

Pistorius alimpiga risasi rafiki yake wa kike Reeva Steenkamp nyumbani kwake Pretoria Februari 2013.