Shambulio jipya la sababisha vifo vya karibu watu 15 Kenya

wakazi walokusanyika mbele ya majengo yaliyoharibiwa na shambulio la Jumapili huko Mpeketoni, Kenya, June 16, 2014.

Washambuliaji wanaodhaniwa ni wanamgambo wa kundi la Al Shabab wamesababisha vifo vya karibu watu 15 katika shambulio jingine siku ya Jumatatu usiku katika eneo la Poromoko katika mji wa Mpeketoni.

Kufuatana na waziri wa ndani Joseph Ole Lenku washambuliaji waliharibu kituo cha mawasiliano cha Safaricom kabla ya kuanza mashambulizi katika lengo la kuwazuia wakazi kuwasiliana na watu wa nje na kutoa onyo.

Tukio hilo linafuatia shambulio la Jumapili katika mji huo huo ambapo watu 48 waliuwawa na wakazi waliokuwa na hasira wanaripotiwa wamekusanyika kwa hasira wakimtaka waziri wa mambo ya ndani anayeaminika yungali katika mji huo kueleza nini kinachotokea.