Afisa wa juu wa jeshi la Nigeria anasema jeshi linajua walipo zaidi ya wasichana 200 ambao wanashikiliwa mateka na wanamgambo w a kiislam na kusema itakuwa vigumu kutumia nguvu kuwaokoa.
Mkuu wa kikosi cha anga cha jeshi Alex Badeh aliwambia waandishi wa habari mjini Abuja jumatatu kwamba operesheni ya kijeshi inaweza kuwa hatari kwa wasichana hao.Akisema “hatuwezi kuuwa wasichana wetu kwasababu ya kutaka kuwaokoa”.
Badeh alisema habari njema kwa wazazi wa wasichana hawa ni kwamba tunajua wapi walipo lakini hatuwezi kuwaambia.
Wasichana hao walitekwa kati kati ya Aprili wakati wakifanya mitihani katika shule ya sekondari huko ndani kabisa katika kijiji cha kaskazini cha Chibok.