MUSCAT OMAN. —
Mkutano wa siku tatu wa Idara ya Elimu na Utamaduni ya Umoja wa Mataifa, UNESCO kuhusu mfumo wa elimu duniani baada ya mwaka wa 2015 umeanza mjini Muscat, Oman Jumanne.
Mkutano huo unahudhuriwa na mawaziri wa elimu pamoja na viongozi wa sekta ya binafsi na mashirika ya kiraia ya nchi wanachama wa UNESCO. Kwenye kikao cha ufunguzi wa mkutano huo, wajumbe walitoa mwito kwa ajili ya mshikamano zaidi kuhusu kuachiliwa kwa wasichana zaidi ya mia mbili wanaoshikiliwa na Boko Haram huko Nigeria.
Mkutano huu unaojumuisha wajumbe zaidi ya mia tano unalenga kuweko na mpango mpya wa mfumo wa elimu duniani, kutokan na kutofanikiwa kwa Malengo ya Milenia kwa ajili ya Maendeleo MDGs ifikapo mwakani. Kwenye sherehe ya ufunguzi wa mkutano huu, Bi. Ann Therese Ndog-Jatta, mwakilishi wa UNESCO kwa Afrika amesema kwamba bado njia ni ndefu kwa bara hilo kufikia elimu bora kwa wote.
Takwimu za Idara ya UNESCO zinaonyesha kwamba kuanzia mwaka wa 2000 hadi sasa watu milioni 17 wa Afrika walipewa mafunzo ya msingi yaani kujua kusoma na kuandika. Lakini bara hilo bado lina asilimia 40 ya vijana wasiojuwa kusoma wala kuandika.
Tatizo jingine kubwa linalozuia maendeleo ya Afrika ni kiwango cha elimu. Nchi nyingi zimetajwa na UNESCO kwamba zimekuwa na mfumo wa bora elimu na siyo elimu bora.
Ikiwa kuna juhudi za kuweko na usawa wa kuwapa elimu wavulana sawa na wasichana, lakini bado waalimu ni lazima kupewa ujuzi zaidi.
UNESCO inaeleza kamba kuna umuhimu wa kuwaachisha kazi walimu milioni tatu na laki saba katika nchi za afrika kusini mwa janga la Sahara, wakati huo huo kuna hitajika kuajiriwa waalimu wapya milioni moja na laki sita.
Walimu ni lazima walipwe mishahara bora ili wao pia watoe elimu bora. Ushelisheli ndio nchi pekee ya Afrika ambayo inafikia MDGS kwenye sekta ya elimu.
Wajumbe kwenye mkutano huu wa Muscat, waliomba kuwepo na mshikamano zaidi kote duniani ili wasichana waliokamatwa na kundi la Boko Haram huko Nigeria warejeshwe kwenye familia zao .
Mkutano huu wa elimu kwa wote uloandaliwa na UNESCO utamalizika alhamisi na utafungwa rasmi na Bi. Irina Bokova kiongozi wa shirika la UNESCO.