Wasikilizaji waashiria amani kudumishwa Afrika 2014 katika "Live Talk"

Wakazi wa mji wa Benni waandamana kulalamika dhidi ya mauwaji ya Kanali Mamadou Ndala Jan, 03 2013

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa waloshiriki katika makala ya "Live Talk", matarajio ya 2014 wamesisitiza haja ya kutanzua migogoro ya Afrika na waafrika wenyewe badala ya kutegemea msaada kutoka mataifa ya nje ya bara hilo.

Wakieleza matarajiyo yao na kujibu maswali ya wasikilizaji, Mohamed Saleh mjini Paris, Hassan Mwakimwako mjini Mombasa na Ismael Mfaoume wamesema migogoro iliyotokea Afrika mwaka 2013 kwa sehemu kubwa inatokana na ukosefu wa utawala bora na uchi wa madaraka kuliko ugomvi wa kikabila.

Your browser doesn’t support HTML5

Live Talk matarajio ya 2014


Bw. Saleh anasema mbali na kuimarisha utawala bora na kupambana na ulaji rushwa nchi za Kiafrika zinabidi kuzingatia zaidi suala la nishati kuhakikisha kuna umeme na maji, kwani bila ya mambo hayo hapawezi kupatikana maendeleo.

Bw Mwakimwako, anasema kutokana na migogoro ya Sudan Kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati na jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo viongozi wa Afrika wanabidi kutafuta suluhisho kati yao na kutosubiri msaada kutoka nje.