Rais Uhuru Kenyatta anajaribu kuzuia kesi yake ICC.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alipokuwa akizungumza na Wakenya wa ng'ambo Disemba 2002.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya anajaribu kuzuia kesi inayoendelea dhidi yake kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC .

Mawakili wa Kenyatta wanasema wana ushahidi wa kutosha juu ya matukio mbali mbali ya ukiukaji wa utaratibu ikiwa ni pamoja na kuwatishia mashahidi . Waliwasilisha maombi ya maandishi mahakamani jana, wakitaka kesi hiyo ifutiliwe mbali.

Rais Kenyatta anataarjiwa kwenda mahakamani Novemba 12. Anakabiliwa na mashitka ya uhalifu dhidi ya uubinadamu kwa shutuma za kupanga njama za ghasia baada ya uchaguzi mwaka 2007 na 2008.

Ghasia hizo zilipelekea zaidi ya watu 1000 kupoteza maisha na kusababisha zaidi ya nusu milioni kupoteza makazi yao.

Kesi ya naibu wake William Ruto inaendelea huko ICC akikabiliwa na tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinadamu.