Madktari wanasema Mandela aonyesha maendeleo mazuri.

Rais mstaafu Nelson Mandela.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anasema shujaa wa ubaguzi wa rangi Nelson Mandela bado ana hali mbaya lakini madakatari wanaona kwamba ameonyesha maendeleo mazuri katika siku mbili zilizopita.

Bw.Zuma alisema Jumapili kwamba rais huyo wa zamani wa Afrika kusini mwenye umri wa miaka 94 anaendelea kuwasiliana na familia yake.

Rais Zuma alitoa taarifa hiyo katika mji wa New Castle katika maandamano ya kuadhimisha uasi wa wanafunzi wa Soweto wa mwaka 1976 wakati wa utawala wa weupe wachache Afrika kusini . Aliwaomba waandamanaji hao kuungana naye kumtakia kheri ya siku ya kina baba duniani.

Bw.Mandela amekaaa hospitali kwa muda wa siku 9 akitibiwa kutokana na maambukizo ya mapafu.