Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini Tanzania imesema kuwa kutakuwepo na makundi mawili ambayo yatapewa fursa ya kuandaa mikutano kujadili rasimu ya katiba mpya.
Maamuzi hayo ya tume ya mabadiliko ya katiba yalitolewa na Jaji mstaafu Joseph Warioba, alipozungumza na vyombo vya habari nchini humo hivi karibuni.
Maamuzi hayo yamepokelewa kwa hisia tofauti na baadhi ya wadau wa mabadiliko hayo ya katiba.
Sauti ya Amerika imezungumza na mwenyekiti wa jukwaa la katiba Bw.Deus Kibanda ambaye ameelezea nia ya asasi yake kuwasilisha kesi mahakamani kuzuia mchakato wa katiba mpya kutokana na mapungufu ambayo tume ya katiba nchini humo imedaiwa kuyafumbia macho.
Ikiwa ni pamoja na elimu kwa wananchi, siasa za vyama na mabaraza ya katiba ambayo inaelezewa hayako huru.

Your browser doesn’t support HTML5