Rais mpya wa Kenya Uhuru Kenyatta ameapishwa katika sherehe ambazo zilihudhuriwa na maelfu ya watu waliokuwa wakishangilia huku wakipunga bendera zao katika mji mkuu Nairobi.
Tukio hilo ni kilele cha uchaguzi wa Machi 4 uliofanyika kwa amani ambapo Kenyata alimshinda Waziri Mkuu anayaeondoka madarakani Raila Odinga . Rais huyo ameahidi kufanya kazi kuboresha maisha ya Wakenya wote.
Viongozi wengine wengi barani Afrika walihudhuria hafla hiyo, ikiwa ni pamoja viongozi wa mataifa ya nchi jirani za Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Baadhi ya mataifa ya magharibi yaliwakilishwa na mabalozi wao wakati wakijaribu kupunguza mawasiliano na rais huyo kutokana na kesi inayomkabili huko ICC.
Wakati wa hotuba katika sherehe za kuapishwa rais wa Uganda Yoweri Museveni aliwapongeza Wakenya kwa kumchagua Bw.Kenyatta na akikaidi kile alichosema kuwa ni kurubuniwa na ICC.
Rais Kenyatta anakabiliwa na mashitaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu kwa shutuma za kusaidia ghasia za baada ya uchaguzi mapema 2008 ambazo zilipelekea vifo vya watu zaidi ya 1,100 na wengine 600,000 kupoteza makazi yao. Kesi yake itaanzwa kusikilizwa mwezi Julai.