Russia yakosoa mshirika wake Syria.

Waziri mkuu wa Russia Dmitry Medvedev.

Russia imetoa moja ya ukosoaji wake mkali dhidi ya rais wa Syria Bashar al- Assad na kusema mshirika wake huyo wa muda mrefu amefanya kosa kubwa kwa kuchelewesha mabadiliko ya kidemokrasia yanayodaiwa na upinzani wa Syria.
Waziri mkuu wa Russia Dmitry Medvedev alisema hayo katika mahojiano na televisheni ya CNN Jumapili . Alisema Bw.Assad alitakiwa kufanya kazi haraka ili kuzungumza na wapinzani wa mrengo wa kati.
Medvedev alisema anaamini nafasi ya rais Assad kubaki madarakani inazidi kuwa haififu, lakini akakariri msimamo wa Russia kwamba hatima ya Syria sharti ibaki mikononi mwa raia wa Syria.

Russia imekuwa ikitoa silaha kwa familia ya Assad kwa muda mrefu na imepinga maazimio ya baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yanayotoa mwito kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati kuzima mzozo nchini humo.