Pagum Amum afanya mazungumzo ya usalama na kiuchumi.

Msuluhishi mkuu wa Sudan Idris Abdel-Qadir akimkaribisha msuluhishi mkuu wa Sudan Kusini Pagum Amum katika uwanja wa ndege wa Khartoum.

Mkuu wa usuluhishi wa Sudan Kusini amekutana na maafisa wa Sudan kwa mazungumzo ya usalama na kiuchumi.

Pagum Amum ameelezea mazungumzo yake ya Jumapili na waziri wa Ulinzi Abdelrahim Mohamed Hussein na afisa wa juu Nafie Ali Nafie kuwa yenye mafanikio lakini hakutoa maelezo zaidi juu ya mazungumzo hayo.

Sudan na Sudan kusini walisaini makubaliano mwezi Septemba kusuluhisha mzozo juu ya ada ambayo kusini inabidi iwalipe Khartoum ili kusafirisha mafuta ghafi kupitia kwenye mabomba yake , maeneo ya kusafishwa na bandari moja huko kaskazini.

Lakini makubaliano hayo hayajaanza rasmi kwa kuwa pande hizo mbili bado zinapingana juu ya kuondoa majeshi kutoka kwenye eneo lenye mzozo.