Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 13:49

Zanzibar yasema tume ya uchaguzi ina mamlaka kamili


Mabango ya kisiasa kwenye ukuta mjini Zanzibar
Mabango ya kisiasa kwenye ukuta mjini Zanzibar

Serikali ya Mapinzuzi Zanzibar (SMZ) imesema kwamba Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ipo huru katika kusimamia na kuendesha mambo yake bila ya kuingiliwa na jumuiya za kimataifa.

SMZ imewataka wananchi wa Zanzibar kujiandae na uchaguzi wa marudio utakaofanyika baada ya kutangazwa kwa tarehe na tume hiyo yenye mamlaka ya kuitisha uchaguzi huo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:04 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ Haji Omar Kheir alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mji mdogo wa Gomani uliopo katika kisiwa cha Tumbatu.

Kauli hiyo aliitoa katika hafla ya kukabidhi msaada kwa familia saba zilizochomewa nyumba moto wakati wa vurugu za uchaguzi Oktoba 25 mwaka huu wa 2015.

Haji amesema uchaguzi wa Oktoba umefutwa na kutangazwa rasmi katika gazeti la serikali, na sasa tume ya uchaguzi inakamilisha taratibu za kurudia uchaguzi mwengine.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar uchaguzi wa Oktoba 25 ulikabiliwa na udanganyifu kinyume na misingi ya demokrasia.

Kuhusu Dk Shein kuendelea kuwepo madarakani amesema kifungu cha 28(1) kinampa uwezo huo pamoja na baraza lake la mawaziri kukaa madarakani licha ya uchaguzi kufutwa.

XS
SM
MD
LG