Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 16:16

Zelenskyy aomba viongozi wanaokutana Uswizi waongeze msaada kwa Ukraine


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akihutubia Kongamano la Kimataifa la Uchumi mjini Davos, Uswizi
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akihutubia Kongamano la Kimataifa la Uchumi mjini Davos, Uswizi

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy Jumanne ameomba viongozi wa kisiasa na kibiashara waliokusanyika kwenye kongamano la Kimataifa la Uchumi mjini Davos, Uswizi, waongeze msaada wao kwa taifa lake, au wahatarishe Russia kushambulia mataifa mengine

Hayo yamejiri wakati kukiwa na wasi wasi huko Kyiv, kwamba vita hivyo vimeanza kuondoka kwenye ajenda kuu ya dunia. Wakati macho yakiwa yameelekezwa kwenye ghasia za Mashariki ya Kati, pamoja na mashambulizi ya wa Houthi, dhidi ya meli za mizigo kwenye bahari ya Shamu, Zelenskyy alitumia kikao cha Davos, kukumbusha ulimwengu kinachohitajika, wakati Ukraine ikiendelea kukabiliana na uvamizi wa Russia.

Hotuba yake ilishangiliwa pakubwa kutoka kwa wajumbe wanaohudhuria kikao hicho, ingawa Ukraine inahitaji zaidi ya kukubalika mbele ya washirika wake. “Tunahitaji kukamata udhibiti wa anga za Ukraine, sawa na tulivyoshika udhibiti wa bahari ya Shamu, Tunaweza hilo,” amesema Zelenskyy. “Washirika wetu wanafahamu kinachohitajika, na kwa viwango gani, ili kuweza kupiga hatua ardhini,” ameongeza Zelenskyy.

Forum

XS
SM
MD
LG