Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 13:19
VOA Direct Packages

Zaidi ya watu 500 wadaiwa kufa Iran, kwenye misako dhidi ya maandamano


Waandamanaji wa Iran kwenye picha ya maktaba.
Waandamanaji wa Iran kwenye picha ya maktaba.

Vikosi vya usalama vya Iran vimeua takriban watu 537 kwenye msako dhidi maandamano yaliyoanza Septemba kulingana na kundi moja la kutetea haki za binadamu likiwa ongezeko kubwa la idadi iliyoripotiwa awali.

Kundi hilo la Iran Human Rights lenye makao yake nchini Norway, pia limeongeza kuwa ingawa watu 4 wamenyongwa ndani ya kipindi hicho kutokana na kushiriki maandamano, wengine zaidi ya 300 wamenyongwa kwa tuhuma tofauti ndani ya kipindi hicho, ikionekana kuwa mbinu ya kukandamiza jamii.

Maandamano ya Iran yalianza katikati mwa Septemba kufuatia kifo cha Mahsa Amini mwanamke wa Kikurdi wa Iran akiwa mikoni mwa polisi, baada ya kukamatwa kwa madai ya kutovalia hijab.

Waandamanaji walitokea barabarani wakiomba kuondolewa kwa sheria kali za mavazi kwa wanawake pamoja na kuondolewa kwa utawala mkali wa kiislamu ambao imetawala taifa hilo tangu 1979.

Idadi kubwa ya vifo imeripotiwa kwenye jimbo la Sistan –Baluchistan kusini mashariki mwa taifa ambako kundi la waliowachache la Baluch Sunni limekuwa likifanya maandamano kila wiki.

XS
SM
MD
LG