Dozi 899,000 za awali za chanjo zimewasili katika nchi 9 barani Afrika ambazo zimeathiriwa sana na ugonjwa wa mpox ambao uko barani humo hivi sasa, Shirika la afya duniani-WHO na taasisi nyingine za afya zilisema siku ya Jumatano.
WHO ilitangaza mpox ni dharura ya afya ya umma duniani kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka miwili hapo mwezi Agosti, baada ya aina mpya ya virusi vinavyoitwa Clade Ib, vilivyosambaa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwenda nchi jirani.
Mwezi Septemba baada ya kukabiliwa na ukosoaji kwamba inachukua hatua za polepole sana kuhusu chanjo, Shirika la Afya Ulimwenguni lilisitisha chanjo ya Bavaria Nordic kwa mpox, na ilisema ilikuwa inaitambua chanjo aina ya LC16, iliyotengenezwa na KM Biologics ya Japani kama chaguo kwa chanjo inayoweza kukabiliana na Mpox.
Forum