Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 03:04

Xi Jinping afanya kikao na Blinken mjini Beijing


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken,(Kushoto) akiwa na rais wa China Xi Jinping mjini Beijing Jumatatu.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken,(Kushoto) akiwa na rais wa China Xi Jinping mjini Beijing Jumatatu.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken Jumatatu amekutana na rais wa China Xi Jinping muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa China Wang Yi, kwa kile wizara yake imekielezea kama kikao kilichokuwa na mafanikio.

Mikutano hiyo imefanyika katika siku ya pili na ya mwisho ya ziara yake huko Beijing, iliyolenga kuimarisha uhusiano wa Marekani na China.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Mathew Miller alisema katika taarifa kwamba Blinken na Wang walizungumzia masuala kadhaa kuhusu mataifa hayo mawili, pamoja na ya kimataifa na pia nafasi za ushirikiano zilizopo katika kukabiliana na changamoto kati ya mataifa yao.

Wizara ya mambo ya nje ya China kupitia taarifa imesema kwamba mkutano kati ya Wang na Blinken umefanyika wakati muhimu wa uhusano kati ya China na Marekani, na kwamba ni muhimu kuimarisha tena uhusiano uliokuwa unadorora.

Forum

XS
SM
MD
LG