Watu takribani bilioni moja duniani wanakabiliwa na hatari ya kupata matatizo ya kusikia au hata kupoteza uwezo wa kusikia kutokana na athari za kelele au sauti kubwa, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la afya ulimwenguni-WHO.
Uchunguzi unaonesha kuwa magogjwa ya masikio yanazidi kuongezeka miongoni mwa jamii hasa watu wanaotumia vifaa vya kuvaa masikioni-ear phone ili kusikiliza muziki kwa sauti ya juu.
Mwandishi wa Sauti ya Amerika-VOA, Josephat Kioko alitembelea maeneo kadhaa katika mji wa Mombasa kusikiza kiwango cha kelele akiwa ndani ya mabasi madogo yanayotoa huduma za abiria ndani ya mji katika eneo moja hadi jingine maarufu kama matatu nchini Kenya.