Rais wa Marekani Joe Biden na mteule wake wa Mahakama ya Juu, jaji Ketanji Brown Jackson watachukua ushindi, kutokea pamoja katika ikulu ya White House.
Hili linafanyika siku moja baada ya Baraza la Seneti kupiga kura 53 kwa 47 kumuidhinisha mwanamke mweusi katika Mahakama ya Juu nchini kwa mara ya kwanza katika historia ya Marekani.
Tukio hili la Ijumaa linatoa fursa kwa Biden kupata uungwaji mkono wa chama chake wakati ambapo utendaji wake ukipata idadi ya chini.
Makamu wa rais Kamala Harris, mwanamke wa kwanza mweusi kushikilia wadhifa huo, pia atajiunga katika sherehe hiyo.
Baraza la Seneti lilimuidhinisha Ketanji Brown Jackson kushika wadhifa katika Mahakama ya Juu jana Alhamisi, na kuvunja kizuizi cha kihistoria kwa kuhakikisha nafasi yake kama jaji wa kwanza mwanamke mweusi na kumpa Rais Joe Biden uidhinishaji wa pande mbili kwa juhudi zake alizoahidi za kubadilisha Mahakama hiyo.
Jackson atachukua kiti chake wakati jaji Stephen Breyer atakapostaafu kipindi cha majira ya joto mwaka 2022, na hivyo kuimarisha mrengo wa kiliberali wa mahakama inayotawaliwa na Wa-Conservative.