Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 22:01

WFP yasema idadi ya watu walio katika shida ya njaa imefikia milioni 45


Mamilioni ya watu wapo katika shida ya njaa ulimwenguni
Mamilioni ya watu wapo katika shida ya njaa ulimwenguni

Kuongezeka kutoka watu milioni 42 mwanzoni mwaka huu kulitokana na tathmini ya usalama wa chakula ambayo iligundua watu wengine milioni 3 wanakabiliwa na njaa nchini Afghanistan, shirika la mpango wa chakula Duniani (WFP) lilisema

Shirika la chakula la Umoja wa Mataifa lilisema Jumatatu kwamba idadi ya watu walio kwenye hali mbaya ya njaa katika nchi 43 imeongezeka hadi milioni 45 huku njaa kupita kiasi ikiongezeka kote ulimwenguni.

Kuongezeka kutoka watu milioni 42 mwanzoni mwaka huu kulitokana na tathmini ya usalama wa chakula ambayo iligundua watu wengine milioni 3 wanakabiliwa na njaa nchini Afghanistan, shirika la mpango wa chakula Duniani (WFP) lilisema.

World Food Program (WFP)
World Food Program (WFP)

Mamilioni ya watu wapo hatarini. Tuna migogoro, mabadiliko ya hali ya hewa na janga la COVID-19 linaloongeza idadi ya watu walio na njaa kupita kiasi, mkurugenzi mtendaji wa WFP, David Beasley alinukuliwa akisema.

Na takwimu za hivi karibuni zinaonyesha hivi sasa kuna zaidi ya watu milioni 45 wanaelekea kwenye njaa, alisema baada ya safari kwenda Afghanistan mahala ambako WFP inaongeza msaada wake kwa karibu watu milioni 23.

XS
SM
MD
LG