Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:53

Waziri wa zamani wa Gambia afikishwa mbele ya mahakama ya Uswizi


Picha ya mahakama aliypelekwa Ousman Sonko Jumatatu, January 8, 2024, mjini Bellinzona, Uswizi
Picha ya mahakama aliypelekwa Ousman Sonko Jumatatu, January 8, 2024, mjini Bellinzona, Uswizi

Waziri wa zamani wa  mambo ya ndani wa Gambia leo amefikishwa mahakamani huko  Uswizi akikabiliwa na mashitaka ya ukatili dhidi ya binadamu, kwa kuhusika kwake katika miaka kadhaa  ya ukandamizaji.

Ukatili huo ulianywa na vikosi vya usalama vya taifa hilo la Afrika Magharibi, dhidi ya wapinzani wa dikteta wa muda mrefu Yahya Jammeh. Makundi ya wanaharakati yamepongeza kesi hiyo dhidi ya Ousman Sonko ambaye alikuwa waziri wa mambo ya ndani, kati ya 2006 na 2016, chini ya utawala wa Jammeh, kama fursa ya kufikia hukumu kwenye mahakama ya kimataifa, inayoruhusu kuendeshwa mashitaka ya ukatili uliotekelezwa kwenye taifa la kigeni.

Sonko mapema Jumatatu alifikishwa kwenye mahakama ya jinai katika kusini wa Bellinzona. Kiongozi huyo alikuwa ameomba hifadhi nchini Uswizi Novemba 2016, lakini alikamatwa miezi miwili baada ya kuingia nchini humo. Ofisi ya wendesha mashitaka nchini Uswizi imesema mashitaka dhidi ya Sonko yaliwasilishwa mwezi Aprili na yanajumuisha ukatili uliotekelezwa wakati wa utawala wa Jammeh wa miaka 16, ambao uligubikwa na ukamataji holela, unyanyasaji wa kingono, pamoja na mauaji ya kiholela.

Forum

XS
SM
MD
LG