Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 09:15

Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin anaelekea Kenya siku ya Jumatatu


Waziri wa ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin
Waziri wa ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin

Kabla ya kuondoka kuelekea Nairobi, Austin aliwashukuru wanajeshi wa Marekani katika kambi ya Lemonnier nchini Djibouti akiangazia  kile alichokiita jukumu lao la “kuvutia sana” katika kuwahamisha wanadiplomasia wa Marekani kutoka Sudan mwezi April

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin anasafiri leo Jumatatu kwenda Kenya kwa mazungumzo na maafisa wa ulinzi kuhusu usalama na kupambana na ugaidi.

Kabla ya kuondoka kuelekea Nairobi, Austin aliwashukuru wanajeshi wa Marekani katika kambi ya Lemonnier nchini Djibouti akiangazia kile alichokiita jukumu lao la “kuvutia sana” katika kuwahamisha wanadiplomasia wa Marekani kutoka Sudan mwezi April. “Kwa kweli kituo hiki ni muhimu sana. Tulisimama tukiwa na uwezo hapa kufuatia mashambulizi ya 9/11 wakati tulipokuwa tukifanya juhudi zetu dhidi ya taasisi zenye msimamo mkali”, Austin alisema.

“Tangu wakati huo, sio tu kwamba eneo hili limetusaidia kufanya hivyo, lakini pia tumeongeza aina ya mambo ambayo tunaweza kuyafanya kutoka eneo hili ikijumuisha baadhi ya mambo ambayo hivi karibuni yalitusaidia kama vile kuwahamisha wanadiplomasia wetu kutoka Sudan.”

Austin siku ya Jumapili alivisifu vikosi vya Somalia kwa kufanya “maendeleo ya kuvutia” katika vita dhidi ya al-Shabab lakini akaonya kuwa kundi hilo la kigaidi bado linaweza “kusafirisha ugaidi nje ya nchi kutoka maeneo yasiyo na mipaka.”

Forum

XS
SM
MD
LG