Tetemeko hilo lililokuwa na nguvu ya 7.8 kwenye vipimo vya rikta kufikia sasa limeua zaidi ya watu 46,000 na kuacha mamilioni bila makao, nchini Uturuki na Syria. Wakati akiwa Uturuki, Blinken amekutana na rais Tayyip Erdogan pamoja na waziri mwenzake wa taifa hilo Mevlut Cavusoglu.
Ziara yake inafuatia ile ya Cavusoglu mjini Washington mwezi uliopita. Marekani na Utruruki ambao wote ni wanachama wa NATO wamekuwa wakishauriana ili kuondoa tofauti zilizopo kusuhu uvamizi wa Russia wa Ukraine pamoja na suala la Sweden na Finland kujinga kwenye muungano huo.
Licha ya matumaini madogo ya kupata manusura kwenye vifusi vya majengo yalioporomoka, timu za uokokozi zimeendelea na shughuli zao ingawa kiongozi wao amesema kwamba huenda zikasitishwa baadaye leo.