Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 06:50

Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza adai polisi wanazembea


Polisi wa London akizuia waandamanaji kwenye mkusanyiko wa Okotoba 19, 2023 kuhusiana na mabadiloko ya hali ya hewa. Picha ya maktaba.
Polisi wa London akizuia waandamanaji kwenye mkusanyiko wa Okotoba 19, 2023 kuhusiana na mabadiloko ya hali ya hewa. Picha ya maktaba.

Waziri wa mambo ya ndani ya Uingereza  Alhamisi amekashifu idara ya polisi kwa kuwa wapole kwa waandamanaji wanaounga mkono Palestina.

Amesema kwamba hilo ni kulinganishwa na makundi mengine ya waandamanaji, na kwa hivyo kuongeza mgogoro wa kisiasa uliyosababishwa na vita kati ya Israel na Hamas.

Kwenye shambulizi lisilo la kawaida dhidi ya polisi, waziri Suella Braveman amesema kwamba idara ya polisi ya London ilikuwa ikizembea katika kuwajibisha uvunjaji wa sheria kutoka kwa waandamanji wanaounga mkono Palestina.

Braveman aliwataja waandamanaji hao wanaoitisha sitisho la mapigano huko Gaza kuwa wenye chuki. Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak yupo kwenye shinikizo la kumfukuza kazi Braveman anayeonekana kuleta migawanyiko kwenye kitengo chenye nguvu ndani ya chama tawala cha Kikonsavative.

Forum

XS
SM
MD
LG