Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 13:26

Wazima moto waendelea kudhibiti moto kwenye jangwa la California


Moto unaoendelea kuchoma hifadhi ya kitaifa ya Mojave California, July 30, 2023.
Moto unaoendelea kuchoma hifadhi ya kitaifa ya Mojave California, July 30, 2023.

Wafanyakazi wa zima moto wakisaidiwa na mvua zinazonyesha wamepiga hatua katika kuudhibiti moto ulioenea kwenye jangwa la California kuelekea Nevada na kutishia miti maalamu inayopatikana huko ya ijulikanayo kama Joshua.

Wafanyakazi hao wamesema kwamba mvua kubwa Jumanne adhuhuri zimesaidia katika kuudhibiti kuenea kwa moto huo. Kufikia Jumatano asubuhi, moto huo ulikuwa umedhibitiwa kwa asilimia 30 baada ua kuenea kwenye hifadhi ya kitaifa ya Mojave jimboni California na kuingia Nevada.

Moto huo ndiyo mkubwa zaidi huko California mwaka huu wakati ukiwa umeteketeza maelfu ya hektari ya mbuga hiyo pamoja na miti nadra ya Joshua. Wataalam wanasema kwamba miti hiyo inayopatikana kwenye jangwa hilo pekee, huenda isimee tena baada ya kuchomeka.

Forum

XS
SM
MD
LG