Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:29

Watu zaidi watekwa Nigeria


Watu wenye bunduki wamewateka dazeni ya watu kutoka kijiji kimoja  kaskazini magharibi mwa Nigeria, kwa mujibu wa wawakilishi wawili wa eneo hilo na vyanzo vya Umoja wa Mataifa.

Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku kadhaa baada ya kutekwa kwa zaidi ya wanafunzi 250 waliokuwa shule katika eneo hilo.

Magenge ya uhalifu yamefanya utekaji wa watu wengi kaskazini mwa Nigeria, yakilenga shule, vijiji, na barabara ambapo hufanikiwa kukamata watu wengi kwa ajili ya kuwaweka rehani.

Utekaji wa Jumanne huko wilaya ya Kajuru katika jimbo la Kaduna, umefanyika wakati vikosi vya usalama vilipokuwa vikiwatafuta wanafunzi ambao walitekwa juma lililopita kutoka shule katika kijiji cha Kuriga kilichopo katika umbali wa takribani kilometa 150.

Kuongezeka kwa kiasi kikubwa kwa utekaji kunaisumbua serekali ya rais Bola ahmed Tinubu, ambayo iliahidi kushughulikia usalama.

Forum

XS
SM
MD
LG