Watu watano, akiwemo mtoto, walijeruhiwa katika shambulio hilo, kulingana na chapisho la Meya Vitali Klitschko kwenye Telegram.
Jeshi la anga la Ukraine limesema shambulio hilo lilikuwa kubwa zaidi la ndege zisizo na rubani tangu kuanza kwa uvamizi wa Russia.
Taarifa ya kijasusi ya Uingereza ilisema Novorossiysk itakuwa eneo bora zaidi mbadala, lakini hatua hiyo itahitaji kuhamisha na kupakia upya makombora na pia itahitaji michakato mipya ya uwasilishaji, uhifadhi, utunzaji na upakiaji.
Mwezi uliopita, Ukraine ilisema kuwa Russia ilikuwa na matatizo ya usafiri na vifaa kwa kurusha makombora kutoka Novorossiysk.
Forum