Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 07:08

Watu wachache wajitokeza kupewa chanjo Somalia


Chanjo ya Astrazeneca ilipowasili Somalia
Chanjo ya Astrazeneca ilipowasili Somalia

Somalia ilipokea dozi 300,000 za chanjo ya Astra Zeneca ya virusi vya corona mwezi Machi lakini, maafisa wa afya wanasema chini ya nusu ya dozi hizo zimetumika. Mamlaka inasema kasi ya polepole to utoaji wa chanjo kunatokana na kufunga wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan na habari potofu kuhusu chanjo yenyewe.

Hospitali ya Banadir mjini Mogadishu ni moja ya vituo kuu vya chanjo katika mji mkuu wa Somalia.

Tangu kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, watu wachache wamejitokeza kupata chanjo, ambayo ni muhimu katika mapambano dhidi ya janga la virusi vya corona duniani.

Dk Ubah Farah ni mkurugenzi wa afya ya familia katika wizara ya afya amesema sababu kuu ambayo ilisababisha kasi ndogo ya chanjo ya COVID-19 ni kufunga katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Pia, maswala yanayohusiana na ripoti ya damu kuganda katika nchi nyingine za Ulaya yalisababisha wasiwasi. Hivyo hivyo, dhana kwamba chanjo inaweza kusababisha utasa.

Kiasi cha Wasomali 130,000 hadi sasa wamepatiwa chanjo lakini dozi zilizobaki muda wake utakwisha baada ya miezi michache ikiwa hazitatumika.

Daktari Abdinassir Ibrahim Moalim ni mkurugenzi wa kituo cha kitaifa cha simu cha COVID-19 katika mji mkuu, Mogadishu. Anasema wamepokea simu 18,000 kwa siku katika miezi miwili iliyopita.

Maafisa wanaandikisha viongozi wa dini ya Kiislamu katika juhudi za kuwashawishi watu zaidi wachukue chanjo hiyo.

Mmoja wa walimu mashuhuri wa kidini katika taifa hilo, Sheikh Abdi-Hayi Sheikh Adam, alisema chanjo hiyo haiingilii Ramadhani.

Maafisa wa afya wanatumai kuwa chanjo zitaongezeka wakati Ramadhani ikimalizika.

XS
SM
MD
LG