Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 07:30

Watu 6 wameuawa kufuatia mzozo kati ya wanajeshi na wanamgambo huko DRC

Ramani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na nchi zilizo jirani nae.
Ramani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na nchi zilizo jirani nae.

Kulingana na shirika la habari la AFP, tukio hilo lilitokea Jumamosi mchana katika kijiji cha Mugerwa, takriban kilomita 15 kutoka mji wa Goma katika mazingira ambayo bado hayajafahamika.

Watu angalau sita wameuawa baada ya mzozo kati ya wanajeshi na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali katika eneo tete mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, vyanzo kadhaa vimesema Jumapili.

Kulingana na shirika la habari la AFP, tukio hilo lilitokea Jumamosi mchana katika kijiji cha Mugerwa, takriban kilomita 15 kutoka mji wa Goma katika mazingira ambayo bado hayajafahamika.

Afisa mmoja wa usalama ambaye aliomba jina lake lisitajwe, alisema kwamba wanajeshi walikuwa na ugomvi na wale wanaoitwa wanamgambo Wazalendo, mzozo ambao ulimalizika kwa mapambano ya risasi. “Walishambuliana kwa risasi katika hali hii ya kutoelewana na kuna watu sita wamefariki na wengine tisa wamejeruhiwa”, afisa huyo wa usalama alisema.

Tukio hilo linakuja baada ya mapigano na waasi wa M23 kuzuka mwezi uliopita na kuvunja miezi kadhaa ya utulivu katika eneo hilo. Kundi linaloongozwa na wa-Tutsi la M23 limeshikilia maeneo mengi tangu lilipoanzisha mashambulizi mwishoni mwa mwaka 2021 na kuwafurusha zaidi ya watu milioni moja kutoka kwenye makazi yao.

Forum

XS
SM
MD
LG