Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 05:17

Watu 6 wakamatwa Serbia kufuatia ghasia miongoni mwa mahamiaji


Wahamiaji kutoka Afghanistan wakipanga foleni kwenye kambi ya Obrenovac, karibu na Belgrade, Serbia, Aug. 31, 2021.
Wahamiaji kutoka Afghanistan wakipanga foleni kwenye kambi ya Obrenovac, karibu na Belgrade, Serbia, Aug. 31, 2021.

Polisi wa Serbia wamekamata watu 6 wakiwa na bunduki za rashasha baada ya ufyatulianaji risasi kati ya wahamiaji karibu na mpaka wa taifa hilo na Hungary, ambapo watu watatu walikufa na mmoja kujeruhiwa.

Polisi wameongeza kusema Ijumaa jioni kwamba walizuilia raia wanne wa Afghanistan, na wawili wa Uturuki, wanaoshukiwa kumiliki bunduki pamoja na vilipuzi kinyume cha sheria.

Haijabainika iwapo watafunguliwa mashitaka kutokana na ufyatuliaji huo wa risasi. Ghasia kati ya makundi ya wahamiaji zilizuka mapema Ijumaa kwenye ghala moja lililopo shambani, karibu na kijiji cha Horgos.

Polisi walifanya msako kwenye ghala hilo na kupata bunduki mbili za rashasha pamoja na risasi. Pia walipata wahamiaji 79 ambao walipelekwa kwenye vituo vya mapokezi, taarifa zimeongeza.

Ripoti za ghasia na vita vya bunduki zimeongezeka katika siku za karubi karibu na mpaka kati ya Serbia na Hungary.

Forum

XS
SM
MD
LG