Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 05:12

Watu 12 wameuawa Ituri nchini DRC


Mashambulizi katika mji wa Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC)
Mashambulizi katika mji wa Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC)

Watu 12, akiwemo mwanajeshi mmoja, na raia 11 wazee, waliuawa katika shambulizi la waasi kwenye jimbo la Ituri, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo vyanzo vya hospitali na mamlaka za kieneo zilisema Alhamis

Watu 12, akiwemo mwanajeshi mmoja, na raia 11 wazee, waliuawa katika shambulizi la waasi kwenye jimbo la Ituri, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo vyanzo vya hospitali na mamlaka za kieneo zilisema Alhamis.

Tumepokea miili 11 ya waathirika wa mauaji katika mkoa wa Lopa huko Djugu. Pia kulikuwa na mwili mmoja wa mwanajeshi, John Katabuka, mkurugenzi wa hospitali kuu ya mkoa aliliambia shirika la habari la AFP.

Wanamgambo wa CODECO walishambulia kijiji cha Tshotsho, Jumatano usiku hadi Alhamis asubuhi. Waliwaua raia 11 kwa mapanga na bunduki akiwemo mwanamke mmoja na wazee, afisa wa eneo hilo Gedeon Dino aliiambia AFP.

Kundi la Cooperative for the Development of Congo (CODECO) ni mojawapo ya makundi ya waasi katika nchi hiyo iliyokumbwa na ghasia na vyanzo vya ndani vilisema mauaji ya hivi karibuni yalikuja kama kulipiza kisasi kwa shambulizi walilofanyiwa na jeshi.

Wapiganaji hawa waliwashambulia raia wasiokuwa na hatia wakati wakikimbia risasi za jeshi, msemaji wa jeshi Luteni Jules Ngongo aliiambia AFP. Kijiji cha Tshotsho, kiko kilomita 30 kutoka mji wa Bunia kwenye jimbo la Ituri.

XS
SM
MD
LG