Mashambulizi hayo yanashukiwa kutekelezwa na wanamgambo, kulingana na ripoti kutoka kwa baadhi ya wakazi waliongea na shirika la habari la AFP Alhamisi.
Wakazi wawili pamoja na kiongozi wa kieneo wa kundi la kujitolea la VDP wamesema kwamba shambulizi hilo lilifanyika kwenye eneo la kaskazini ya kati mwa taifa.
Afisa wa VDP amesema kwamba washambuliaji wengi walizimwa na wapiganaji wa kujitolea baada ya makabiliano ya takriban saa mbili. Burkina Faso ambalo ni taifa la Sahel limekuwa likikabiliana na wanamgambo kwa miaka 7, wengi wao wakitokea kwenye nchi jirani ya Mali.