Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:02

Watoto watumika kama wapiganaji Mali, mapigano yaendelea Ethiopia


Mwanajeshi apita karibu na mtoto wakati anapiga doria nchini Mali. March 25, 2019.
Mwanajeshi apita karibu na mtoto wakati anapiga doria nchini Mali. March 25, 2019.

Ripoti ya mashirika ya kibinadamu yakiongozwa na shirika la umoja wa mataifa la kuwashughulikia wakimbizi UNHCR, imenakili visa 230 vya Watoto kusajiliwa na makundi ya wapiganaji katika miezi sita ya kwanza yam waka 2020, ikilinganishwa na visa 215 mwaka 2019.

Mashirika hayo pia yamesema kwamba Watoto 6,000 wengi wao wakiwa wavulana, wanafanya kazi katika machimbo ya dhahabu.

Msaidizi wa mkuu wa UNHCR Gillian Triggs, amesema kwamba vita na hali mbaya ya uchumi kutokana na janga la Corona katika eneo la Sahel imesababisha ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu eneo hilo.

Amesema kwamba Watoto wanasafirishwa kimagendo, kunajisiwa, kuuzwa, kulazimishwa kufanya ngono au kulazimishwa kuoa na kuolewa.

Mapigano yaendelea Ethiopia

Wataalam wameonya kwamba vita vya Ethiopia ambavyo vimedumu karibu mwezi mmoja, huenda vikageuka na kuwa mzozo usiomalizika.

Onyo hilo linajiri wakati jeshi la Ethiopia limetangaza ushindi baada ya kutwaa mji mkuu wa Mekele katika eneo la Tigray.

Mapigano hayo ya tangu Novemba 4, yanaripotiwa kusababisha vifo vya maelfu ya watu.

Maelfu ya watu wamekimbilia Sudan kama wakimbizi.

Mamilioni ya watu wa Tigray wanaripotiwa kuwa katika matatizo makubwa kufuatia vita hivyo na janga la virusi vya Corona.

Kuna ripoti kwamba mapigano bado yanaendelea kati ya vikosi vya Tigray na wanajeshi wa Ethiopia.

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameshutumu vikosi vya Tigray kwa kushambulia kambi ya jeshi la Ethiopia.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG