Watanzania wasmeadhimisha miaka 50 tangu pale marais Hayati Mwalimu Julius Nyerere wa Tanganyika na Hayati Abedi Amani Karume wa Zanzibar kutia saini hati ya kunganisha nchi hizi mbili hapo April 22 1964.
Kumbukumbu zinaeleza kwamba makubaliano hayo yaliidhinishwa na kuwa sheria baada ya mabunge ya mataifa hayo mawili yani bunge la Tanganyika na baraza la mapinduzi la Zanizbar kuidhisha mkataba April 24 1964.
Sherehe kubwa za kuunganisha mchanga wa nchi hizo zilifanyika na tangu wakati huo nchi hizo zimekua ni moja, na jjna rasmi lililokubalika kuanzia Oktoba 28 1964 ilikua Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hata hivyo, upinzani haujapata kukosekana kwa kitu chechote kipya, basi tangu wakati huo kumekuwepo na upinzani kutoka zanzibar hadi kufikia hii leo wakati wa kuadhimisha miaka 50 ya muuungano, mjadala mkubwa nchini humo ni juu ya mageuzi ya katiba. Suala kuu linalojitokeza ni aina ya muungano kuwepo baada ya miaka hii hamzsini.
Tume maalum ya katiba imewahoji wananchi na kutayarisha rasimu inayopendekeza muundo wa serikali tatu lakini chama tawala cha CCM kinapinga jambo hilo na kushikilia mfumo wa serikali mbili..
Wachambuzi wetu, Dk, Mwesiga Baregu mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba, Dk. Bashiru Ally na Dk. Ayub Riyoba wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Harith Ghasani mwandiwshi wa kitabu "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru", Dk. Ali Taarab wa Konde Pemba, wachambuzi wa kisiasa Hamza Zuberi na Mohamed Said wanazungumzia juu ya mafanikio, changamoto na mustakbal wa Mungano huo katika majadiliano yanayofuata.