Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 07:59

Wataalam wa afya wakutana Botswana ili kujadili baadhi ya changamoto zilizopo barani Afrika


Wataalam wa afya wakiwa kwenye mkutano wa awali, Botswana.
Wataalam wa afya wakiwa kwenye mkutano wa awali, Botswana.

Zaidi ya wataalam 1,000 wa afya wakiwemo mawaziri kutoka mataifa ya Afrika wanakutana Botswana kwa mkutano wa kikanda wa Shirika la kimataifa la Afya, WHO.

Wanaohudhuria wanalenga kuhakikisha kwamba Afrika imejiandaa vilivyo kutokana na majanga katika siku za nyuma, kinyume na ilivyokuwa wakati wa janga la corona.

Akihutubia mkutano wa siku 5 ulioanza Jumatatu, mkuu wa kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa cha WHO barani Afrika Jean Kaseya amesema kwamba kuna umuhimu wa Afrika kuwa tayari kukabiliana na majanga, hasa baada ya konyesha mapungufu wakati wa janga la Covid-19.

Wakati wa Covid, Afrika ilikuwa na changamoto ya kutoa chanjo kwa watu wake kutokana na kutoweza kununua chanjo za kutosha, wakati chini ya asilimia 10 ya wakazi wakiwa wamechanjwa.

Mkuu wa WHO Tedros Ghebreyesus amesema kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yameongeza changamoto za kiafya barani humo.

Forum

XS
SM
MD
LG