Washukiwa wanajihadi walishambulia kambi ya kijeshi katikati mwa Mali siku ya Jumamosi maafisa wawili wa kieneo waliochaguliwa na chanzo kimoja cha kidiplomasia wameliambia shirika la habari la AFP, wakielezea eneo hilo kama kambi ya Russia.
Utawala wa Mali mwaka 2022 ulianza kufanya kazi na kile inachokiita wakufunzi wa kijeshi wa Russia. Wapinzani wanasema hawa ni mamluki kutoka kundi la Wagner. Hatuna idadi kwa hivi sasa hali bado inachanganya, ni wanajihadi ambao waliulenga uwanja wa ndege na kambi ya Russia iliyo karibu nao, afisa aliyechaguliwa wa eneo hilo aliliambia shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina.
Maafisa wawili wa jeshi la Mali pia wamethibitisha kuwa shambulio hilo limetokea katika mji wa Sevare, katika mkoa wa Mopti.