Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:04

Warnock na Walker mshindi kujulikana baadae jimboni Georgia


Herschel Walker (L) mgombea wa Republican na Raphael Warnock wa Democratic. Nov. 10, 2022, Atlanta, Georgia.
Herschel Walker (L) mgombea wa Republican na Raphael Warnock wa Democratic. Nov. 10, 2022, Atlanta, Georgia.

Matokeo ya kinyang'anyiro cha Jumanne yataamua ikiwa Democrats wana wingi wa moja kwa moja wa viti 51-49 vya Seneti au kudhibiti baraza hilo kwa viti sawa 50-50 kutokana na kura ya makamu rais Kamala Harris

Wapiga kura wa jimbo la Georgia nchini Marekani wanatarajiwa Jumanne kuamua mchuano wa mwisho wa kiti cha baraza la seneti nchini humu wakichagua kati ya Seneta wa Chama cha Democratic Raphael Warnock na mchezaji wa zamani wa football ya Marekani wa Chama cha Republican Herschel Walker katika duru ya pili ya uchaguzi. Uchaguzi wa Jumanne unakamilisha kampeni za wiki nne zilizoshuhudia wimbi la wanasiasa na fedha kutoka nje ya jimbo hilo pamoja na kuongezeka mashambulio ya masuala ya kibinafsi.

Duru hiyo ya pili ya mwaka huu huko Georgia haina umuhimu mkubwa ikilinganishwa na mbili za mwaka 2021, wakati ushindi wa Warnock na mwenzake wa chama cha Demokratik huko Georgia, Jon Ossoff ulipowapatia Democrats udhibiti wa Seneti. Matokeo ya kinyang'anyiro cha Jumanne yataamua ikiwa Democrats wana wingi wa moja kwa moja wa viti 51-49 vya Seneti au kudhibiti baraza hilo kwa viti sawa 50-50 kutokana na kura ya Makamu Rais Kamala Harris.

Uchaguzi huo wa duru ya pili unaleta mapambano makali kati ya Warnock, seneta wa kwanza mweusi wa jimbo hilo na kiongozi mwandamizi wa kanisa la Atlanta, ambako Martin Luther King Jr alihubiri, na Walker, nyota wa zamani wa mpira wa football wa Chuo Kikuu cha Georgia na mwanasiasa chipukizi ambaye anaungwa mkono na rais wa zamani Donald Trump.

XS
SM
MD
LG