Eneo hilo takatifu, kwa Wayahudi na Waislamu, mara nyingi limekuwa kitovu cha machafuko kati ya Israel na Palestina, mkvutano ilikuwa tayari imeongezeka huku kukiwa na wimbi la ghasia za karibuni. Mapigano katika eneo hilo mwaka jana yalichangia kuzusha vita vya siku 11 kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas huko Ukanda wa Gaza.
Mapigano hayo yanakuja wakati nyeti sana. Ramadhani mwaka huu inaambatana na Pasaka, likizo kuu ya Kiyahudi ya wiki nzima inayoanza leo Ijumaa wakati wa machweo ya jua, na wiki takatifu ya wakristo, ambayo kilele chake ni Jumapili ya Pasaka. Sikukuu hizo zinatarajiwa kuleta maelfu ya waumini katika Jiji la Kale la Jerusalemu, makao kwa maeneo makuu matakatifu kwa dini zote tatu.