Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:13

Wanajihadi wa Boko Haram wamewauwa wafugaji 17 Nigeria


Mfano wa kundi la wanamgambo wa Boko Haram wa nchini Nigeria
Mfano wa kundi la wanamgambo wa Boko Haram wa nchini Nigeria

Wanamgambo hao siku ya Jumamosi waliwashambulia wafugaji waliokuwa wanalinda ng’ombe wao  katika malisho karibu na kijiji cha Airamne katika wilaya ya Mafa, wanamgambo hao walisema

Wanajihadi wa Boko Haram waliwaua wafugaji 17 na kuiba mifugo yao kufuatia mapigano katika jimbo lenye matatizo kaskazini mashariki mwa Nigeria la Borno wanamgambo wanaojilinda wenyewe wameliambia shirika la habari la AFP Jumatatu.

Wanamgambo hao siku ya Jumamosi waliwashambulia wafugaji waliokuwa wanalinda ng’ombe wao katika malisho karibu na kijiji cha Airamne katika wilaya ya Mafa, wanamgambo hao walisema.

"Wafugaji kumi na saba waliuawa katika mapigano na ng’ombe wao wote kuchukuliwa," kiongozi wa wanamgambo Babakura Kolo alisema.

Mwanamgambo mwingine, Ibrahim Liman, alitoa idadi hiyo hiyo.

Alisema wanajihadi hao walianzisha shambulizi kutoka kambi zilizo karibu na msitu wa Gajiganna, ambako walihamia baada ya kulazimishwa kuondoka katika ngome yao katika msitu wa Sambisa na wapinzani wao wa kijihadi ISWAP na jeshi la Nigeria.

Kundi la Islamic State West Africa Province (ISWAP) lilijitenga na Boko Haram mwaka 2016 na liipanda na kuwa kundi kubwa katika machafuko ya muda mrefu ya wanajihadi katika eneo hilo.

Liliteka maeneo mengi chini ya udhibiti wa Boko Haram baada ya kiongozi Abubakar Shekau kuuawa katika mapambano na ISWAP mwezi Mei mwaka 2021.

Kundi la Boko Haram na ISWAP yamezidi kuwalenga raia hasa wakataji miti, wakulima na wafugaji, wakiwashutumu kwa kuwapeleleza kwa ajili ya jeshi na wanamgambo wa ndani dhidi ya wanajihadi.

XS
SM
MD
LG