Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 22:49

Wanajeshi wanne wa Tunisia wamefariki kwa ajali ya ndege


Ramani ya Tunisia na nchi zilizo jirani nae
Ramani ya Tunisia na nchi zilizo jirani nae

Akitoa rambirambi zake kwa familia zilizofiwa, rais alisema katika mkutano na Waziri wa Ulinzi Imed Memmiche kwamba ajali hiyo ilisababisha vifo vya wanajeshi wanne, kulingana na taarifa rasmi. Awali wizara ya ulinzi ilizungumzia kuhusu miili miwili iliyopatikana baharini

Wanajeshi wanne wa Tunisia wamefariki wakati helikopta ya kijeshi ilipoanguka baharini kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, Rais Kais Saied alisema Alhamisi, akisisitiza umuhimu wa kukarabati vifaa vya kijeshi.

Akitoa rambirambi zake kwa familia zilizofiwa, rais alisema katika mkutano na Waziri wa Ulinzi Imed Memmiche kwamba ajali hiyo ilisababisha vifo vya wanajeshi wanne, kulingana na taarifa rasmi. Awali wizara ya ulinzi ilizungumzia kuhusu miili miwili iliyopatikana baharini.

Wizara hiyo inasema mawasiliano yalipotea na helikopta ambayo ilikuwa ikifanya safari ya usiku katika mji wa Cape Serrat siku ya Jumatano jioni ikiwa na wafanyakazi wane ndani ya ndege. Jeshi la Tunisia limepoteza ndege kadhaa katika mafunzo au operesheni za uchunguzi katika miaka ya hivi karibuni.

Forum

XS
SM
MD
LG