Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 19:50

Wanajeshi wa Ufaransa wataondoka Niger ifikapo Disemba 22; Anasema Macron


Mojawapo ya vifaa vya jeshi la Ufaransa katika operesheni zake mjini Niamey huko Niger. Oct. 10, 2023.
Mojawapo ya vifaa vya jeshi la Ufaransa katika operesheni zake mjini Niamey huko Niger. Oct. 10, 2023.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza kuwa vikosi hivyo vitaondoka ifikapo mwishoni wa mwaka huu, ambapo kikosi cha kwanza kimeondoka nchini humo mwezi Oktoba. “Ifikapo Desemba 22, wanajeshi wote wa Ufaransa pamoja na vifaa vyao watakuwa wameondoka Niger”

Kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa wanaoshiriki katika operesheni ya kupambana na wanajihadi nchini Niger kutakamilika ifikapo Desemba 22, jeshi la nchi hiyo ya Sahel limesema Jumanne.

Watawala wa kijeshi wa Niger walifuta makubaliano ya ulinzi na Ufaransa, mshirika wake wa jadi wa usalama, wakati uhusiano ulipoharibika kufuatia mapinduzi ya mwezi Julai.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza kuwa vikosi hivyo vitaondoka ifikapo mwishoni wa mwaka huu, ambapo kikosi cha kwanza kimeondoka nchini humo mwezi Oktoba. “Ifikapo Desemba 22, wanajeshi wote wa Ufaransa pamoja na vifaa vyao watakuwa wameondoka Niger” jeshi limesema katika taarifa.

Kuondoka kwao hadi sasa kumefanywa kwa njia iliyoratibiwa na salama, iliongeza. Kulingana na vyombo vya habari vya Niger, wanajeshi 1,346 wa Ufaransa na asilimia 80 ya vifaa vyao wameondoka, huku wanajeshi 157 pekee ndio wapo.

Forum

XS
SM
MD
LG