Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:33

Wanajeshi kumi wa Niger wauwawa karibu na mpaka wa Mali


Wanajeshi wa Niger washika doria kwenye jangwa. Oct. 29, 2019.
Wanajeshi wa Niger washika doria kwenye jangwa. Oct. 29, 2019.

Waziri wa ulinzi wa Niger Alkassoum Indattou amesema Jumamosi kwamba takriban wanajeshi 10 wa Niger wameuwawa huku wengine zaidi ya darzeni wakijeruhiwa .

Tukio hilo ni kufuatia shambulizi la kushtukiza lililofanywa na washambuliaji waliokuwa na silaha karibu na mpaka wa taifa hilo la Sahel linalopakana na Mali.

Takriban watu 16 hawajulikani walipo kufuatia shambulizi hilo la Ijumaa jioni katika mji wa Banibangou ulioko karibu na Mali .Indattou ameongeza kusema kwamba msaada wa jeshi la anga uliwalazimisha washambuliaji kukimbia na kuvuka mpaka na kuingia nchini Mali.

Niger pamoja na jirani zake Mali na Burkina Faso wanajitahidi kuwazima waasi wanaohusishwa na makundi ya kigaidi ya al Qaida na Islamic State ambao mara kwa mara wanafanya mashambulizi kwenye eneo kubwa la Sahel.

XS
SM
MD
LG