Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 07:50

Wanadiplomasia wa juu wa India na China wakutana pembeni mwa kikao cha ASEAN, Jakarta, Indonesia


Kikao cha mawaziri wa mambo ya nje kutoka mataifa ya ASEAN mjini Jakarta, Indonesia
Kikao cha mawaziri wa mambo ya nje kutoka mataifa ya ASEAN mjini Jakarta, Indonesia

Wanadiplomasia wa juu kutoka India na China wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja pembeni ma mkutano wa ASEAN unaofanyikia Jakarta, Indonesia.

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi, amemwambia mwenzake wa India Subrahmanyam Jaishankar kwamba mataifa yote mawili yanahitaji kuimarisha ushirikiano wao kulingana na nakala ya wizara ya mambo ya nje ya China.

Wang alimwambia Jaishankar,” Mataifa yote yanahitaji kushirikiana na kutekeleza mambo pamoja, na wala siyo kumalizana au kushukiana.” Mataifa hayo yanashirikiana mpaka mrefu ambako kumekuwa na mivutano kati ya majeshi yao, lakini mikataba kadhaa kuhusu mpaka imeanza kuimarisha mahusiano.

Mwaka 2020, wanajeshi kutoka mataifa yote mawili walishambuliana, wakati wanajeshi 20 wa India walipoteza maisha , pamoja na wanne kutoka China. Wizara ya mambo ya nje ya China imesema kwamba India imekubali kufanya mazungumzo zaidi kuhusu mizozo ya mpakani. India ndiye mshirika wa pili wa kibiashara wa China sasa hivi.

Forum

XS
SM
MD
LG