Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 15:41

Wakimbizi 29 wafariki Tanzania kwa kipindupindu


Wakimbizi wa Burundi wakiwa eneo la Kagunga, Tanzania, May 17, 2015.
Wakimbizi wa Burundi wakiwa eneo la Kagunga, Tanzania, May 17, 2015.

Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu umeuwa wakimbizi 29 wa Burundi ambao walikimbilia nchini Tanzania kuepuka ghasia za kisiasa nchini mwao.

Shirika la kuhudumia wakimbizi katika Umoja wa Mataifa-UNHCR lilisema Ijumaa kwamba raia wawili wa Tanzania pia walifariki kutokana na mlipuko huo ambao uliwaathiri watu 3,000 katika eneo la Kagunga karibu na ziwa Tanganyika. Maafisa wamepeleka maji safi, madawa na vifaa vingine ili kuzuia kusitisha mlipuko huo.

Wakimbizi wa Burundi, April 10, 2015.
Wakimbizi wa Burundi, April 10, 2015.

UNHCR ilisema kesi mpya 300 hadi 400 za mlipuko wa kipindupindu zinaripotiwa kila siku katika eneo la mpaka wa Tanzania mahala ambako kuna wimbi kubwa la wakimbizi kutoka Burundi.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, zaidi ya raia wa Burundi 64,000 walikimbilia nchini Tanzania katika wiki za karibuni wakikhofia machafuko ya kisiasa. UNHCR na marafiki zake walijitokeza kuomba msaada hapo Ijumaa wakisema dola milioni 207 zinahitajika ili kujibu matatizo ya kibinadamu yaliyosababishwa na msongamano wa wakimbizi. Maelfu kadhaa ya raia wa Burundi pia wamekimbilia nchini Congo na Rwanda.

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza

Wakati huo huo Rais Pierre Nkurunziza aliripotiwa kucheza soka Alhamis huku waandamanaji wakiandamana katika mitaa nchini humo. Wakosoaji wa bwana Nkurunziza wanasema muhula wa tatu anaotaka kuwania kiongozi huyo utakiuka katiba ya Burundi inayoruhusu kiongozi kuwepo madarakani kwa mihula miwili. Wafuasi wake wanaeleza kwamba muhula wa tatu unaruhusiwa kwa sababu Nkurunziza alichaguliwa na bunge sio wapiga kura kwenye mhula wake wa kwanza madarakani hapo mwaka 2005.

XS
SM
MD
LG