Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 03:56

Mshindi wa uchaguzi wa rais Kenya atajulikana kesho: IEBC


Wawakilishi wa vyama wasubiri matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa rais katika uwanja wa Bomas Nairobi Kenya
Wawakilishi wa vyama wasubiri matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa rais katika uwanja wa Bomas Nairobi Kenya
Ikiwa imebaki saa chache kabla ya kutangazwa matokeo rasmi ya uchaguzi wa rais Kenya, bado haijulikani ikiwa Uhuru Kenyatta ataweza kupata asilimia 50 na kura moja kunyakua ushindi katika duru ya kanza.

Wakuu wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC walisema mchana wa Ijuma kwamba ingawa matokeo yanatolewa pole pole lakini wanauhakika Wakenya watapata matokeo rasmi usiku wa Ijuma kama walivyoahidi hiyo jana.

Wakiwa wameshatangaza matokeo ya wilaya 252 za uchaguzi kati ya 291, Uhuru Kenyatta anaongoza akiwa na kura 5, 418, 291 ikiwa sawa na asili mia 49.72, huku mpinzani wake wa karibu Raila Odonga ana kura 4, 689,997 sawa na asili mia 43.

wagombea wngine wa kiti cha rais wameanza kukubali kushindwa, Peter Kenneth aliwashukuru wafuasi wake walomunga mkono na kusema yuko tayari kufanya kazi na mtu yeyoter atakae shinda.

Musalia Mudavadi, mgombea kiti cha rais wa mungano wa AMANi alyetarajiwa kuwaletewa changamoto kubwa Uhuru na Raila alitangaza mapema Ijumaa kwamba kutokana na hesabu ni wazi mashindano ni kati ya mafahali wawili na anasubiri matokeo ya mwisho.
XS
SM
MD
LG