Wakazi wa Marekani pia huenda wakaangazia uchaguzi ujao wa rais wa Marekani utakaofanyika baadaye mwaka huu. Siku kuu hiyo ya Jumatatu inaadhimishwa ikiwa ni siku 100 tangu Oktoba 7, pale Hamas walipofanya shambulizi kusini mwa Israel na kuuwa takriban watu 1,200, huku wengine takriban 240 wakichukuliwa mateka.
Tangu wakati huo, zaidi ya mateka 100 wa Israel bado wanashikiliwa mateka, huku zaidi ya wapalestina 23,000 wakiuliwa kwenye mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza. Mashirika ya kimataifa ya afya yameonya kwamba hali ya kibinadamu kwenye eneo hilo inaendelea kuwa mbaya sana.
Waandaji wa sherehe za Martin Luther King Jr wamemsihi Rais Joe Biden kuitisha sitisho la kudumu la amani huko Gaza na Ukingo wa Magharibi. Pia wameomba kuachiliwa kwa mateka wote wa Israel pamoja na wafungwa wa kivita wa Palestina. Wameomba pia kusitishwa mara moja kwa misaada ya kifedha kwa jeshi la Israel kutoka Marekani.
Forum