Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 02:02

Wanaharakati washambulia mgahawa mwengine Mogadishu


Watu wakimsaidia msichana aliyejeruhiwa katika shambulio la kujitioa mhanga kwenye mgahawa mashuhuri "The Village". Novemba 3, 2012.
Watu wakimsaidia msichana aliyejeruhiwa katika shambulio la kujitioa mhanga kwenye mgahawa mashuhuri "The Village". Novemba 3, 2012.
Wajitoa mhanga wawili wamejaribu kushambulia mgahawa mmoja unaomilikiwa na Muingereza mwenye asili ya ki-Somali mjini Mogadishu Jumamosi mchana.

Mashahidi wameiambia Sauti ya Amerika kwamba watu wanne ikiwa ni pamoja na washambuliaji hao wawili waliuliwa katika miripuko miwili mikubwa karibu na mgahawa unaojulikana kama “The Village.”

Mlinzi aliyewazuia washambulizi kuingia katika jengo hilo aliuliwa pamoja na raia moja, watu wengine 10 walijeruhiwa. Mgahawa huo ni maarufu na kutumiwa zaidi na maafisa wa serikali, waandishi habari na wanasiasa.

Hapo mwezi wa Septemba wajitoa mhanga wawili walishambuliwa mgahawa mwengine unaomilikiwa na mwenye mgahawa wa “The Village” katika mji mkuu na kuwauwa watu 15.

Kikosi cha kulinda amani cha umoja wa afrika amisom huko Somalia kinasema kinadhani wanaharakati wa al shabab walihusika na shambulizi la mwezi wa septemba.
XS
SM
MD
LG