Wahisani wa kimataifa watakutana mwezi ujao huko Geneva Uswissi kuzungumzia kuongezeka kwa janga la kibinadamu katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na ukosefu wa fedha kwa watu milioni 13 walio na shida kubwa ya chakula.
Mahitaji ya kibinadamu yaliosababishwa na mizozo ya ndani yameongezeka mara mbili katika mwaka uliopita mkuu wa huduma za kibinadamu wa umoja wa mataifa Mark Lowcock aliwaambia wanachama wa baraza la usalama Jumatatu.
Umoja wa mataifa unatarajia kupata ahadi ya dola billioni 1.7 kwa mwaka huu ikiwa ni karibu mara nne kwa kiasi kilichoombwa mwaka 2017 katika mkutano wa ahadi wa Aprili 13.
Kutopata fedha za kutosha ni moja ya mambo yanayoturudisha nyuma katika juhudi zetu za misaada ya kibinadamu huko DRC alisema Lowcock.