Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 13:10

Wafanyakazi waliogoma Ufaransa wamevuruga huduma za umma


Wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi wanaandamana nchini Ufaransa kupinga marekebisho ya pensheni
Wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi wanaandamana nchini Ufaransa kupinga marekebisho ya pensheni

Serikali ya Rais Emmanuel Macron ilipendekeza kuongeza umri wa kustaafu kwa ajili ya kulipwa  pensheni kamili uwe kutoka miaka 62 hadi 64 ikisema hatua hiyo ni muhimu ili kuuwezesha mfumo huo ujipange vyema

Wafanyakazi waliogoma nchini Ufaransa kupinga mapendekezo ya marekebisho ya pensheni walivuruga huduma za usafiri, shule na usambazaji umeme leo Alhamisi.

Serikali ya Rais Emmanuel Macron ilipendekeza kuongeza umri wa kustaafu kwa ajili ya kulipwa pensheni kamili uwe kutoka miaka 62 hadi 64, ikisema hatua hiyo ni muhimu ili kuuwezesha mfumo huo ujipange vyema.

Vyama vya wafanyakazi nchini Ufaransa vinapinga mabadiliko hayo na vimependekeza kodi kwa matajiri wakubwa kama njia mbadala.

Huduma za treni na baadhi ya safari za ndege zilifutwa Alhamisi. Asilimia 70 ya walimu wa shule za awali na msingi walisema wanapanga kutofanya kazi, huku wafanyakazi wanaotoa huduma zinazohitaji umeme wanasema watapunguza usambazaji wa huduma hiyo kupinga mabadiliko yaliyopendekezwa.

XS
SM
MD
LG